Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kesi ya Charles Taylor yaanza rasmi Hague

Kesi ya Charles Taylor yaanza rasmi Hague

Mawakili wa utetezi wa mtuhumiwa Charles Taylor, aliyekuwa raisi wa Liberia, wameanza kumtetetea mshitakiwa hii leo mjini Hague, Uholanzi kwa kusisitiza mtuhumiwa hajahusika na mauaji yalioendelezwa na waasi wa Sierra Leone wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoshtadi nchini mika ya nyuma, na wala hajahusika na vitendo vya kujamii kimabavu raia au kulemaza watu wasio hatia.

 Taylor, kiongozi wa awali wa KiAfrika kushtakiwa na mahakama ya kimataifa, ametuhumiwa makosa 11, yakijumlisha kuua, kutesa, udhalilishaji wa kijinsia, utumwa wa kiasherati, na kutumia watoto chini ya umri wa sheria kupigana na kueneza vitisho nchini. Taylor anatazamiwa kujitetea binafsi Ijumanne kwenye kesi inyofanyika sasa hivi mjini Hague, Uholanzi.