Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi vya Serikali Usomali vyapatiwa msaada ziada wa walinzi amani wa UA dhidi ya wapiganaji wapinzani

Vikosi vya Serikali Usomali vyapatiwa msaada ziada wa walinzi amani wa UA dhidi ya wapiganaji wapinzani

Kadhalika, imeripotiwa walinzi amani wa Umoja wa Afrika waliopo Mogadishu, waliingilia kati, kwa mara ya kwanza, moja kwa moja, mapigano kwa madhumuni ya kuvisaidia vikosi vya Serikali kupambana na makundi ya wapinzani.

Msemaji wa vikosi vya UA, aliwaambia waandishi habari kwamba wanajeshi wao walilazimika Ijumapili kutumbukia kwenye mapigano kwa sababu kambi zao zilitishiwa kuhujumiwa na majeshi ya mgambo ambayo yalikuwa yakisogelea eneo la Mogadishu kaskazini. Alisisitiza vikosi vya UA vililazimika "kuendeleza mapigano haya kwa muda mfupi" kwa sababu wanajeshi wake walikabiliwa na hatari ya mashambulio ya wapinzani wa Serikali ya Usomali.