Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa G-8 wameahidi msaada wa kilimo wa $20 bilioni kwa nchi masikini

Viongozi wa G-8 wameahidi msaada wa kilimo wa $20 bilioni kwa nchi masikini

Viongozi wa Kundi la G-8 waliokutana kwenye mji wa L\'Aquila, Utaliana kabla ya kuhitimisha kikao chao waliahidi kuchangisha dola bilioni 20 za kuzisaidia nchi masikini kuhudumia kilimo, ili waweze kujitegemee chakula kitaifa badala ya kutegemea misaada ya kutoka nchi za kigeni, hali ambayo ikidumishwa itasaidia kukomesha duru la umaskini na hali duni.

Ahadi hii ilitolewa manmo siku ya mwisho ya kikao cha viongozi wa Kundi la G-8 na ilikaribishwa na mashirika kadha ya UM.  Jacques Diouf, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO), ambaye vile vile alihudhuria Mkutano wa G-8, alinakiliwa akisema "msaada wa chakula ni kadhia muhimu sana kwa zile nchi masikini ambazo, kwa sasa,  vile vile zimezongwa na matatizo ya ukame, mafuriko, fujo na vurugu, na husumbuliwa sana na tatizo la chakula cha kunusuru maisha."