Skip to main content

Biashara ya silaha ndogo ndogo imeongezeka maradufu ulimwenguni katika 2009, inasema ripoti

Biashara ya silaha ndogo ndogo imeongezeka maradufu ulimwenguni katika 2009, inasema ripoti

Toleo la 2009 la Ripoti ya Uchunguzi juu ya Silaha Ndogo Ndogo Kimataifa limethibitisha biashara ya silaha hizi, pamoja na ile ya silaha nyepesi, iliongezeka kwa asilimia 28 ulimwenguni katika kipindi cha baina ya miaka ya 2000 mpaka 2006.

Huu ni muongezeko wa dola milioni 653 wa biashara halali ya silaha ndogo ndogo na silaha nyepesi, ikijumlisha pia biashara ya spea, vifaa vidogo vidogo na risasi. Kwa mujibu wa ripoti muongezeko mkubwa huu uligundulikana katika usafirishaji wa spea na vifaa vidogo vidogo vyengine vinavyotumiwa kwenye bastola, hali ambayo ilizidi maradufu.