Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kofi Annan ameikabidhi ICC bahasha ya ushahidi juu ya fujo Kenya kufuatia uchaguzi

Kofi Annan ameikabidhi ICC bahasha ya ushahidi juu ya fujo Kenya kufuatia uchaguzi

Luis Moreno Ocampo, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama ya UM juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) leo amepokea kutoka Kofi Annan, Mwenyekiti wa Tume ya UA ya Watu Mashuhuri wa KiAfrika, bahasha iliofungwa yenye ushahidi kuhusu wazalendo waliohusika na vurugu liliofumka Kenya mnamo mwisho wa 2007 na mwanzo wa 2008, kufuatia matokeo ya uchaguzi mkuu nchini humo.

Hali ya Kenya ilikuwa ikichunguzwa tangu 2008, kwa ukaribu zaidi, na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya ICC. Wiki iliopita, baada ya ziara ya ujumbe wa hadhi ya juu wa serikali ya Kenya kwenye ofisi ya ICC iliopo Hague, Uholanzi wadau husika wote pamoja na makundi yaliohasimiana, walikubaliana kusukuma mbele mpango wa amani na juhudi za upatanishi na kuhakikisha fujo na hali ya machafuko hayatoibuka tena nchini mwao. Ocampo alinakiliwa akisema barua aliopokea kutoka Kofi Annan ni moja ya juhudi ya ushirkiano utakaohakikisha haki itatekelezwa bila kuchelewa kwa wakosa wa machafuko Kenya na kuzuia jinai hiyo kutukia kwa siku zijazo.