Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usomali inazingatiwa tena na Baraza la Usalama

Usomali inazingatiwa tena na Baraza la Usalama

Asubuhi Baraza la Usalama lilikutana kwenye kikao cha hadhara kusailia hali, kijumla, katika Usomali hususan shughuli za kulinda amani za AMISOM.

Naibu KM juu ya Masuala ya Kisiasa, B. Lynn Pascoe kwenye risala aliowakilisha kwenye kikao alitilia mkazo umuhimu kwa walimwengu kufanya kila wawezalo kuhakikisha Serikali ya Mpito ya Usomali (TFG) haitoanguka, kwa masilahi ya jumuiya nzima ya kimataifa. Naibu KM juu ya Misaada ya Vifaa vya Kilojistiki juu ya Operesheni za Amani za UM, Susana Malcorra, yeye alielezea kwenye taarifa yake kuhusu maendeleo ya hatua, ya idara yake, katika kuhudumia kihali na mali vikosi vya Umoja wa Afrika kwa Usomali (AMISOM), mchango ambao anaamini utawawezesha wanajeshi huko kuendesha operesheni zao kwa mafanikio. Wakati huo huo aliyahimiza mataifa wanachama kutimiza mchango wao walioahidi siku za nyuma kuhusu operesheni za amani katika Usomali.