Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamisheni ya CAC inazingatia mabadiliko ya kudhibiti kemikali zinazodhuru kwenye chakula

Kamisheni ya CAC inazingatia mabadiliko ya kudhibiti kemikali zinazodhuru kwenye chakula

Kamisheni iliobuniwa bia na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), yaani Kamisheni ya CAC (the Codex Alimentarius Commission) kutathminia vipimo juu ya usalama wa vyakula, imetangaza vipimo 30 vipya vitakavyotumiwa kimataifa kuongoza ukaguzi juu ya usalama wa chakula duniani.

Kwa mfano, moja ya kipimo kipya kitakachotumiwa kutekeleza tathmini hiyo kinaambatana na juhudi za kuzuia na kupunguza athari za kemikali zenye madhara, kwa afya, zinazozalishwa na mafuta ya kupikia yanayotumiwa kukaanga vyakula vilivyojaa kabohidrati (carbohydrate) kama chipsi (mbatata za/viazi vya kukaanga), biskuti na mikate.