Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA imeteua Mkurugenzi Mkuu mpya

IAEA imeteua Mkurugenzi Mkuu mpya

Bodi la Utawala la Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) lenye wajumbe 35, ambalo linakutana hivi sasa kwenye mji wa Vienna, Austria leo limemteua Balozi Yukiya Amano wa Ujapani kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa taasisi hii ya kimataifa.

Katika duru ya mwisho ya kura, Balozi Amano alipata kura 23 za wawakilishi wa Bodi la IAEA, wakati mgombea wa pili, Abdul Samad Minty wa Afrika Kusini alipata kura 11, na mjumbe mmoja wa Bodi la Utawala aliamua kutopiga kura. Balozi Amano atamrithi Mohamed El Baradei, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa IAEA tangu 1997, ambaye atakamilisha muda wake wa kazi tarehe 30 Novemba mwaka huu.