Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza kuu lapitisha azimio linalolaani vikali mapinduzi ya Honduras

Baraza kuu lapitisha azimio linalolaani vikali mapinduzi ya Honduras

Ijumanne alasiri Baraza Kuu la UM lilipitisha azimio liliolaani vikali mapinduzi haramu ya serikali yaliofanyika Honduras, taifa liliopo Amerika ya Kati.

Azimio limetoa mwito wa kimataifa unaopendekeza kurudishwa, haraka, madarakani kiongozi wa taifa aambaye aliteuliwa kwa utaratibu wa kidemokrasia, yaani Raisi José Manuel Zelaya Rosales. Kwa kufuatana na taarifa za vyombo vya habari, Raisi Zelaya aliondoshwa madarakani kimabavu na wanajeshi Ijumapili iliopita, saa chache tu kabla ya kura ya maoni kufanyika juu ya uwezekano wa kurekibisha katiba ya taifa.  Azimio la Baraza Kuu la UM, liliopitishwa kwa sauti, na bila ya kupingwa, lilisisitiza mapinduzi yaliotokea Honduras "yamekatiza mfumo wa kikatiba na kidemokrasia nchini na kuharamisha haki halali ya utawala." Raisi wa Honduras Zelaya, alipohutubia Baraza Kuu hapo jana, alipokelewa kwa makofi ya pongezi kutoka wawakilishi wote wa Mataifa Wanachama, waliokuwa wamesimama kuonyesha ushikamano wao juu ya uhalali wa utawala wake.