Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ameingiwa wasiwasi juu ya mripuko wa vurugu Honduras

KM ameingiwa wasiwasi juu ya mripuko wa vurugu Honduras

KM Ban Ki-moon ametangaza taarifa ilioelezea kuwa na wasiwasi kuhusu mtafaruku uliozuka katika taifa la Honduras, la Amerika ya Kati ambapo inasemekana Raisi José Manuel Zelaya Rosales aliondoshwa madarakani kwa nguvu majuzi.

KM alisisitiza hatua hiyo ni haramu na ilikwenda kinyume na maadili ya taasisi za kidemokrasia ziliopo nchini humo. Alisema anapinga kabisa uhalifu wa kumshika Raisi wa Honduras aliyeteuliwa kikatiba. KM alisisitiza "wawakilishi wote waliochaguliwa kwa mfumo wa kidemokrasia Honduras, na wale walioondoshwa nje ya katiba, kisheria wanawajibika warejeshwe, halan, kwenye madaraka." Alisema haki za binadamu nchini humo nazi pia ni lazima kuhishimiwa, ikijumlisha haki ya kumpatia Raisi Zelaya, aila yake na wawakilishi wa serikali halali hifadhi na usalama." Aliwataka raia wa Honduras wote kushiriki, kwa njia za amani na moyo wa upatanishi, kwenye zile juhudi za kutatua mzozo uliokabili taifa lao kwa sasa. Aliahidi KM ya kuwa UM upo tayari kuchangisha kila msaada unaohitajika kuukamilisha kwa njia ya amani mzozo wa kikatiba katika Honduras.