Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa BK juu ya Mzozo wa Kifedha na Uchumi Duniani waendela New York

Mkutano wa BK juu ya Mzozo wa Kifedha na Uchumi Duniani waendela New York

Mkutano Mkuu juu ya Mzozo wa Uchumi na Fedha Duniani na Athari Zake Kwa Maendeleo umeingia siku ya pili Alkhamisi ya leo, ambapo wawakilishi wa kutoka karibu nchi 150 wanaendelea kujadilia uwezekano wa kusuluhisha mizozo hii kwa "maamuzi yatakayokuwa na natija, kwa kiasi kikubwa, na kwa muda mrefu, miongoni mwa umma wa kimataifa."

Mnamo siku ya kwanza ya mkutano, kwenye majadiliano yaliofanyika Ijumatano ya jana, wawakilishi wa kutoka nchi kadha wa kadha zinazoendelea, walilalamika kwenye risala zao, ya kuwa uchumi wa kimataifa ulioporomoka, ikichanganyika na mzozo wa kifedha, pamoja na kupungua kwa malipo ya fedha zinazoingia nchini kutoka raia waliopo nje, ni mambo yaliozusha athari mbaya kabisa kwenye mataifa yao, licha ya kuwa nchi hizi masikini hazihusiki kamwe na matatizo ya uchumi na kifedha yaliopamba, katika kipindi cha karibuni, kwenye soko la kimataifa.