Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNODC inajiandaa kutangaza ripoti ya 2009 juu ya tatizo la madawa ya kulevya duniani

UNODC inajiandaa kutangaza ripoti ya 2009 juu ya tatizo la madawa ya kulevya duniani

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) litawakilisha Ijumatano ripoti mpya kuhusu tatizo la madawa ya kulevya ulimwenguni katika 2009.

Ripoti inasema licha ya juhudi mbalimbali zilizofanyika katika nchi nyingi kudhibiti madawa ya kulevya, huduma ambazo pia ziliendelezwa na washirika kadha wa kimataifa, tatizo la uzalishaji wa madawa haya ulimwenguni, pamoja na matumizi haramu, ikichanganyika na magendo ya bidhaa hizi, imethibitishwa vitendo hivi vinaendelea kuzusha vizingiti dhidi ya utulivu na usalama wa umma wa kimataifa, kwa ujumla.