Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UN-HABITAT atunukiwa "Tunzo ya Goteberg"

Mkuu wa UN-HABITAT atunukiwa "Tunzo ya Goteberg"

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Makazi (UN-HABITAT), Anna Tibaijuka, ametangazwa kuwa ni mmoja wa washindi watatu wa Tunzo ya Göteberg, kwa michango yao ya kitaifa na kimataifa, katika maamirisho ya huduma ya maendeleo yanayosarifika.

Tunzo ya Göteberg hufananishwa na "Tunzo ya Nobel kwa Mazingira", na itakabidhiwa washindi husika mnamo mwezi Novemba, kwenye mji wa Göteberg, Uswidin. Washindi wawili wengine waliofanikiwa kuteuliwa kupokea Tunzo ni pamoja na Enrique Pelosa, aliyekuwa meya wa mji wa Bogota, na pia Soren Hermansen, wa kutoka Denmark - ambaye mwaka 2008 alitambuliwa na Gazeti la Time la Marekani kuwa kama ni 'Shujaa wa Mataifa katika Kutunza Mazingira.