Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya ya wahamiaji dhidi ya UKIMWI inazingatiwa na bodi la UN-AIDS,linalokutana rasmi Geneva

Afya ya wahamiaji dhidi ya UKIMWI inazingatiwa na bodi la UN-AIDS,linalokutana rasmi Geneva

Bodi la la Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) limeanza rasmi Geneva kikao cha 24, kilichokusudiwa kuzingatia mahitaji ya umma unaohama hama, ukijumuisha wahamaji na wahamiaji wa ndani na nje ya mataifa yao.

Mkutano ulihutubiwa, kwa mara ya awali, na Mkurugenzi Mkuu mpya wa UNAIDS, Michel Sidibé, ambaye alisema kwenye taarifa yake siku hizi kuna mwelekeo mpya wa uhamiaji kimataifa, hali ambayo imeonyesha dalili ya kuwa na utata mkubwa. Kwa hivyo, alisema, ni muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kujaribu kuhakikisha wahamiaji wote, kwa ujumla, huwa wanapatiwa uwezo wa kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI, pamoja na kupatiwa matibabu na uangalizi unaofaa utakasaidia kudhibiti bora maradhi haya. UM umezihimiza nchi wanachama kujitahidi kuhakikisha idadi ya wahamiaji, hasa wale walio dhaifu kihali na mali, huwa wanapokea misaada kutoka mashirika ya baina ya serikali, ili kudhibiti vyema hatari ya maambukizi ya VVU kwenye maeneo yao.