Skip to main content

Kilimo hujiokoa zaidi na mizozo ya kiuchumi kushinda sekta nyenginezo, inasema ripoti ya FAO/OECD

Kilimo hujiokoa zaidi na mizozo ya kiuchumi kushinda sekta nyenginezo, inasema ripoti ya FAO/OECD

Ripoti ya pamoja iliotolewa na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), iliowakilishwa rasmi Ijumatano, imeeleza kwamba ilivyokuwa uchumi wa kimataifa hautarajiwi kufufuka na kuota mizizi ya kuridhisha mpaka baada ya miaka miwili/mitatu ijayo, wataalamu wanaashiria mporomoko wa muda wa bei za bidhaa za kilimo kimataifa utakuwa wa wastani.

Ripoti ilisisitiza ya kuwa chakula ni kitu cha lazima, kimsingi, kwa umma; kwa hivyo, huduma za kilimo, zinazoambatana na chakula, hujaaliwa uwezo mkubwa wa kustahamili marekibisho yanayoletwa na mizozo ya uchumi iliopamba duniani kwa sasa hivi, kushinda shughuli nyenginekwa sababu mahitaji yake ni makubwa. Kwa mujibu wa fafanuzi za ripoti hiyo, bei za chakula kwa mwaka huu, ziliteremka kutoka kilele kilichofikiwa mnamo mwanzo wa 2008. Hata hivyo, bei hizo bado ni za kiwango cha juu katika nchi masikini. Kwa hivyo ripoti Imehadharisha, katika miongo ijayo hakuna dalili zenye kuonyesha bei za bidhaa za kilimo itarejea kima kilichokuwepo kabla ya mzozo wa kiuchumi kufumka katika soko la kimataifa. Kwa kulingana na bayana hiyo, ripoti imetoa mwito kwa Mataifa Wanachama kuchangisha misaada ziada inayofaa, pamoja na kubuni sera mpya zitakazoziwezesha nchi maskini, kuwekeza  kwenye miundombinu, na kwenye utafiti wa mifumo ya kuimarisha shughuli za maendeleo, kwa kuhakikisha pia wakulima watapatiwa motisha utawaowawezesha kutumia ardhi na maji kwa uadilifu wenye natija ya muda mrefu.