Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Dunia Kupiga Vita Kuenea kwa Jangwa

Siku ya Dunia Kupiga Vita Kuenea kwa Jangwa

Tangu 1995 UM unaihishimu tarehe 17 Juni, kila mwaka, kuwa ni Siku ya Kupiga Vita Kuenea Kwa Jangwa. Ripoti za UM juu ya tatizo la kueneza majangwa, kutokana na matumizi badhirifu ya ardhi, inaashiria watu milioni 200 watalazimika kuhama makazi katika mwaka 2050 kutakakosababishwa na mabadiliko ya katika mazingira.

Tafiti za UM zimethibitisha dhahiri kwamba uharibifu wa ardhi ulimwenguni, unahatarisha utulivu wa kitaifa na kikanda, hasa ilivyokuwa thuluthi moja ya tabaka la Dunia sasa hivi linaathiriwa na tatizo la kuenea kwa jangwa. Hali hii inaashiriwa kuukosesha umma wa mataifa husika, njia za kujipatia riziki, na vile vile huzorotisha huduma za maendeleo, na inakadiriwa itaathiri kihali watu bilioni moja ziada katika dunia. Kwa mujibu wa risala ya KM, tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa ni moja ya mambo yenye kuchochea jangwa kuenea kwa kasi katika ulimwengu. Lakini Achim Steiner, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mzingira (UNEP) aliripoti kuwa kumeandaliwa miradi maalumu na taasisi yake, yenye matumaini makubwa ya kurekibisha matatizo ya kuenea kwa majngwa na kudhibiti vyema uharibifu wa ardhi, hasa katika bara la Afrika. Miradi hii, alisema, imeshatekelezwa kwa majaribio katika baadhi ya mataifa Afrika, na imeanza kutoa natija za kuridhisha. Alitoa mfano wa miradi ya UNEP iliotumiwa katika mataifa tisa ya Afrika, kufufua aina ya majani yaliotoweka siku za nyuma, kwa kutumia maji yanayotokana na mvua ya kuvuna; na pia ule mradi wa kuendeleza malisho ya mifugo kwa zamu pamoja na miradi mengine kama hiyo.