Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uongozi mpya unahitajika kukabiliana na mizozo ya ajira duniani. inasema ILO

Uongozi mpya unahitajika kukabiliana na mizozo ya ajira duniani. inasema ILO

Juan Somavia, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) alipohutubia kikao cha ufunguzi wa Mkutano Mkuu juu ya Masuala ya Mizozo ya Ajira Duniani, uliofanyika Geneva, amependekeza kuwepo “uongozi mpya katika viwango vyote vya kiuchumi na kijamii" ili kusuluhisha vyema mizozo ya ajira kimataifa. Mkuu huyo wa ILO, alisema ulimwengu hauwezi tena kusubiri uchumi ukuwe, kwanza, kwa miaka kadha kabla ya kuamua kuzalisha ajira.

Alisema ufufuaji wa dharura wa ajira, kwa lengo la kutunza mahitaji ya kijamii, ni hali ambayo ambayo lazima kupewa umuhimu wa hali ya juu, wakati kunaandaliwa sera za umma na makubaliano ya kibiashara. Somavia, alisisitiza, uchumi wa katika soko la kijamii utayarishwe kwa taratibu zitakazosaidia kuzuia kuzuka tena ile hali ya ubadhirifu uliokiuka mipaka, na tofauti za kimatabaka, zilizopamba kimataifa kwenye siku za nyuma.