Maendeleo kupatikana kwenye mkutano wa kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

12 Juni 2009

Mkutano wa UM uliofanyika Bonn, Ujerumani mwezi huu, kuzingatia masuala yanayohusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani, umemalizika Ijumaa ya leo na iliripotiwa kumepatikana mafanikio ya kuridhisha katika maandalizi ya waraka wa ajenda ya majadiliano, kwa kubainisha dhahiri matarajio ya serikali wanachama kutoka Mkutano ujao wa Copenhagen, ili kuharakisha udhibiti bora wa taathira za mabadiliko ya hali ya hewa kimataifa.

Wajumbe kutoka nchi 183 walikusanyika Bonn, Ujerumani hasa kuzingatia waraka wa usuluhishi utakaotumiwa kuongoza majadiliano ya kubuni mkataba mpya utakaoidhinishwa kwenye kikao cha Copenhagen, kitakachofanyika mwezi Disemba.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud