Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS kuuzindua umma wa kimataifa, VVU ni washiriki bubu wa maafa ya dharura

UNAIDS kuuzindua umma wa kimataifa, VVU ni washiriki bubu wa maafa ya dharura

Mumtaz Mia, mshauri wa Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) kwa ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, amenakiliwa akitahadharisha ya kwamba mara nyingi, hasakatika mataifa yanayoendelea, huduma ya kuzuia maambukizo ya virusi vya UKIMWI huwa haipewi umuhimu unaostahiki, hasa baada ya kuzuka mizozo kadhaa ya dharura katika majiraya karibuni.

Alikumbusha kwamba "kinga ya maambukizo ya VVU ni huduma muhimu sana kuendelezwa na mataifa husika, kwa sababu ina uwezo mkubwa wa kuokoa maisha ya umma, kwa muda mrefu ujao" na ni suala linalohitaji kupewa umbele na itiko la dharura na nchi hizo.