UNAMID imepoteza mlinzi amani Darfur

UNAMID imepoteza mlinzi amani Darfur

Askari wa Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) ameripotiwa kufariki Ijumatano, kufuatia ajali ya gari katika Nyala, mji mkuu wa Darfur Kusini, baada ya kukamilisha doria ya kulinda raia kieneo.

Ripoti ya UNAMID ilisema askari huyo alianguka kutoka kwenye gari wakati wakikaribia kambi yao, iliokuwepo kilomita 5 kutoka eneo la ajali. Askari huyo - ambaye uraia wake bado haujatangazwa, ikisubirwai kuarifiwa familia yake - alipelekwa kwenye hospitali ya UNAMID haraka kwa matibabu, lakini bahat imbaya walipowasili huko, alitaganzwa asiye na uhai tena. UNAMID imeanzisha uchunguzi rasmi juu ya tukio hili.