Skip to main content

Treky wa Libya ateuliwa kuwa raisi wa 64 wa Baraza Kuu

Treky wa Libya ateuliwa kuwa raisi wa 64 wa Baraza Kuu

Dktr Ali Abdessalaam Treky wa Jamhuri ya Kiarabu ya Libya, aliye Katibu wa Masuala ya Umoja wa Afrika taifani mwao, amechaguliwa leo na wajumbe wa kimataifa, na bila kupingwa, kuwa raisi wa kikao kijacho cha 64 cha Baraza Kuu la UM, kikao ambacho kitaanza shughuli zake mwezi Septemba (2009).

Kwenye hotuba ya kuukubali wadhifa huo, Dktr Treky alisema atajitahidi kufanya kila linalohitajika kisheria kuhakikisha "shughuli za UM na mashirika yake zinaimarishwa kama inavyostahiki", na alitumai atapata ushirikiano unaofaa kutoka wanachama wote wa UM. Aliahidi kuwa hatofungamana na makundi ye yote yaliopo katika UM isipokuwa yale "yenye upendeleo wa kuimarisha usalama, haki na amani ya jamii nzima ya kimataifa."