Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Udhamini wa Utajiri wa Baharini

Siku ya Udhamini wa Utajiri wa Baharini

Tarehe ya leo, Juni 08, inaadhinmishwa na UM kuwa ni ‘Siku ya Kudhibiti na Kutunza Utajiri wa Baharini’.

Mnamo siku hii, Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limechapisha kitabu muhimu, cha mwongozo wa kiufundi, wenye lengo la kuisaidia sekta ya uvuvi kupunguza athari mbaya dhidi ya aina ya samaki wanaopatikana kwenye kina kirefu cha bahari, na pia kusaidia kutunza ikolojia ya bahari kuu. Mwongozo huu utaziwezesha nchi wanachama kuwa na uwiano mzuri zaidi, katika kuongoza shughuli za uvuvi kinga wa kitaifa, na kwenye maeneo yenye kina kirefu, nje ya mamlaka yao, na kuhakikisha wale samaki wanaochukuwa muda mrefu kuzalishwa, huwa wanahifadhiwa dhidi ya uvuvi wa kihorera, uliokosa mipangilio.