Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM kupongeza risala ya Raisi wa Marekani kukuza uhusiano mwema na ulimwengu wa Waislam

KM kupongeza risala ya Raisi wa Marekani kukuza uhusiano mwema na ulimwengu wa Waislam

KM Ban Ki-moon, kwa kupitia msemaji wake, ameripotiwa kuipongeza hotuba ya Raisi Barack Obama wa Marekani, alioiwakilisha kwenye Chuo Kikuu cha Cairo Alkhamisi ya leo, ambapo alizingatia uhusiano mpya baina ya Marekani na mataifa ya KiIslam. .

KM alisema risala ya Raisi wa Marekani ilimhamasisha, kwa uzito mkuu, hasa ule ujumbe uliosisitiza kuwepo ushirikiano wa kuridhisha kati ya nchi za KiIslam na Marekani, ili kuimarisha amani, mafahamiano na kusuluhisha suitafahaumu zao. Alisema mtazamo huu wa Marekani unawakilisha hatua muhimu katika kuziba mfarakano na mataifa ya KiIslam, na kuendeleza mafahamiano mema ya kuvumiliana kitamaduni, sawa na maadili ya Mkataba wa UM.