Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO inasema akiba ya chakula duniani imetulia mwaka huu

FAO inasema akiba ya chakula duniani imetulia mwaka huu

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetoa ripoti yenye kuashiria mavuno ya nafaka, na akiba ya chakula kwa mwaka huu, hayatodhurika kiuchumi katika soko la kimataifa, kama ilivyotukia katika 2008, ambapo bei ya juu ya chakula ilisababisha mtafaruku na hali ya hatari kimataifa.

Kwa mujibu wa FAO, bei za chakula kwa sasa, bado ni za viwango vya juu katika mataifa mengi yanayoendelea, na uwezo wa watu maskini kupata chakula unaendelea kuhatarishwa kwa sababu ya ukosefu wa mapato, ajira na athari nyengine zinazoletwa na mgogoro wa uchumi wa dunia. Hata hivyo, ilisisitiza FAO, katika 2009 bei za bidhaa za kilimo, kwa ujumla, zilishuhudiwa kuteremka, kwenye maeneo hayo, hususan bei za nafaka.