Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisa wa MONUC anafafanua binafsi maana ya 'Sikukuu ya Walinzi Amani'

Ofisa wa MONUC anafafanua binafsi maana ya 'Sikukuu ya Walinzi Amani'

Tarehe 29 Mei huadhimishwa na UM kuwa ni 'Sikuu ya Kuwakumbuka Walinzi Amani wa Kimataifa' waliochangisha ujuzi wao, na wengine hata kujitoleea mhanga wakati waliposhiriki kwenye zile huduma za kulinda amani, katika kanda mbalimbali za dunia zilizoghumiwa na migogoro, fujo, vurumai na vurugu. Taadhima za mwaka huu zililenga zaidi mchango wa watumishi wa kimataifa wa kike kwenye opersheni za amani za UM.

Christine Kapalata, Afisa Mkuu wa Masuala ya Kisiasa na Shirika la Ulinzi Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUC) karibuni alifanya mahojiano na mtayarishaji vipindi wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM, AZR. Kwenye mazungumzo haya Ofisa wa MONUC alibainisha hisia zake binafsi, na fafanuzi halisi juu ya mchango wa wanawake kwenye operesheni za kulinda amani za UM ulimwenguni.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.