Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma za kilimo ni muhimu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani: FAO

Huduma za kilimo ni muhimu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani: FAO

Juhudi za kufarajia maendeleo yanayosarifika kwenye sekta ya kilimo, hasa katika nchi zinazoendelea, ndio kadhia muhimu pekee yenye uwezo wa kudhibiti bora mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa duniani, na katika kupunguza njaa na ufukara, imeeleza Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO).

Taarifa hii iliwakilishwa kwenye majadiliano kuhusu udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, yanayoendelezwa sasa hivi, kwenye mji wa Bonn, Ujerumani. FAO ilisisitiza kwamba kilimo kikikuzwa kwa utaratibu unaosarifika, kwenye mataifa yanayoendelea, kadhia hii itasaidia pakubwa kupunguza idadi ya watu wanaosumbuliwa na njaa, ambao jumla yao kwa sasa ni bilioni moja; hali ambayo vile vile itasaidia kuongeza mapato kwa wakulima na kuwapatia fursa ya ajira katika mataifa masikini.