Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa dhidi ya matumizi ya tumbaku- 31 Mei 2009

Siku ya kimataifa dhidi ya matumizi ya tumbaku- 31 Mei 2009

Tarehe 31 Mei, ambayo mwaka huu itaangukia Ijumapili, huadhimishwa kila mwaka na UM, kuwa ni Siku ya Upinzani Dhidi ya Matumizi ya Tumbaku Ulimwenguni.

Nasaha ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mwaka huu inazihimiza serikali zote wanachama, kuamrisha vipakti na vifurushi vyote vya bidhaa zinazotengenezewa tumbaku, vijumlishe ilani ya maonyo na tahadhari - na kutumia hata maelezo ya picha - ili kuonyesha hatari ya maradhi na maumivu kwa mwanadamu, yanayoletwa na matumizi ya tumbaku, kama vile matumizi ya sigara. Mada ya taadhima za mwaka huu za Siku ya Kupinga Matumizi ya Tumbaku imesisitiza zaidi juu ya umuhimu wa kutekeleza miradi inayohitajika, kidharura, kukomesha usambazaji wa matumizi ya tumbaku kimataifa, hasa matumizi ya sigara.