Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA itafadhilia JKK na Sudan msaada wa CERF kuwahudumia waathirika wa mashambulio ya LRA

OCHA itafadhilia JKK na Sudan msaada wa CERF kuwahudumia waathirika wa mashambulio ya LRA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imetangaza kutenga dola milioni 10.2 kutoka Mfuko wa UM wa Maafa ya Dharura au Mfuko wa CERF, ili kuisaidia JKK kuhudumia kihali umma ulioathirika na mashambulio ya waasi wa kundi la LRA.

Shirika la miradi ya chakula, WFP, litabarikiwa dola milioni 6.4 kuhudumia umma muathirika; UNICEF itagaiwa dola milioni 1.1 kushuhgulikia huduma za watoto, FAO itapokea dola milioni 1.1 na UNHCR itafadhiliwa dola milioni 1.1. Kadhalika, Sudan inatazamiwa kufadhiliwa dola milioni 15 kutoka Mfuko wa CERF, kuhudumia kihali wakazi 100,000 wa Sudan Kusini waliodhurika na mashambulio ya waasi wa Uganda wa kundi la LRA.