Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumko wa fujo Usomali waitia wasiwasi ICRC kuhusu usalama wa umma

Mfumko wa fujo Usomali waitia wasiwasi ICRC kuhusu usalama wa umma

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC) imeeleza kuwa na wasiwasi kuhusu uharibifu mkubwa ulioshuhudiwa kuzuka karibuni katika Usomali, hali ambayo imeathiri sana hali ya kiutu ya raia walionaswa kwenye mazingira ya mapigano, hususan kwenye mji wa Mogadishu.

Tangu mwanzo wa mwezi Mei, ICRC ilisema, darzeni za watu waliuawa, na mamia ya raia walijeruhiwa pamoja na maelfu kadhaa wengine walilazimika kuhajiri makazi, ili kuepukana na mapigano yalioshtadi kwenye mji wa Mogadishu. Kwa mujibu wa ICRC, asilimia kubwa ya wahamiaji ni wanawake na watoto wadogo, ambao wamelazimika kuyahama mastakimu yao na kujiunga na mamia elfu ya wahamiaji wengine waliokusanyika kwenye makazi ya muda, nje ya mji wa Mogadishu. Wahamiaji hawa wote, inasema ICRC, wanahitajia misaada ya kihali ya dharura kunusuru maisha.