Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtumishi wa UM kutoka Tanzania anazungumzia maana halisi ya "Sikukuu ya Walinzi Amani wa Kimataifa" pamoja na mchango wa wanawake

Mtumishi wa UM kutoka Tanzania anazungumzia maana halisi ya "Sikukuu ya Walinzi Amani wa Kimataifa" pamoja na mchango wa wanawake

Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM imeandaa kipindi maalumu kuiadhimisha \'Sikukuu ya Walinzi Amani wa Kimataifa\' kwa 2009, makalailiokusudiwa kubainisha mchango wa vikosi vya wanajeshi, polisi na watumishi raia katika kuimarisha utulivu na amani duniani.

Tarehe 29 Mei huadhimishwa kila mwaka na UM, kuwa ni siku maalumu ya kuwakumbuka watumishi wenzetu wa wa kimataifa, waliojumuisha michango  kadha wa kadha, kwenye operesheni za amani za UM, zilizotawanyika kwenye sehemu mbalimbali za dunia yetu. Mada ya taadhima za mwaka huu, imemurika zaidi mchango wa wanawake, kwa ujumla, katika kuimarisha usalama na amani ya kimataifa, na umuhimu wa kuwapatia akina mama madaraka zaidi kwenye operesheni za UM, madaraka yatakayowawezesha kuendeleza shughuli zao kwa mafanikio ya kuridhisha.

Mtayarishaji vipindi, wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM, Abdillahi Z. Rijal, wiki hii alipata fursa ya kufanya mazungumzo na mmoja wa maofisa wa kike, kutoka Tanzania, anayetumikia hivi sasa Shirika la Ulinzi Amani la UM katika JKK (MONUC), anayeitwa Christine Kapalata. Yeye ni Afisa Mkuu wa Masuala ya Kisiasa na shirika hili la MONUC.  Kwenye mahojiano hayo, alitupatia mawazo ya binafsi, kuhusu uzoefu aliokusanya katika huduma zakulinda amani.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.