Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID imeripoti hali tulivu imefunika Darfur kwa sasa

UNAMID imeripoti hali tulivu imefunika Darfur kwa sasa

Shirika la Operesheni za Mchanganyiko za UM-UA kwa Darfur (UNAMID) limeripoti Ijumatano kwamba hali ya usalama kwenye eneo hilo, kwa sasa hivi, ni shwari.

Ijumanne UNAMID iliwajibika kuwahamisha watu 19 waliojeruhiwa katika mapigano yaliofumka majuzi katika eneo la Umm Barru liliopo Darfur Kaskazini, na kuwapeleka kwenye vituo vya afya kupata matibabu . Vikosi vya UNAMID vile vile viliripotiwa Ijumanne kufanya doria za kijeshi 69, wakati askari polisi nao pia waliendeleza doria 85 zilizokuwa na lengo la kuhakikisha usalama wa raia. Wakati huo huo, maofisa wa polisi 40 kutoka Sierra Leone waliwasili kwenye mji wa El Fasher, kujiunga na shughuli za operesheni za kulinda amani za UNAMID katika Darfur.