Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ECA inahimiza uwekezaji katika kilimo ili kuzalisha ajira Afrika

ECA inahimiza uwekezaji katika kilimo ili kuzalisha ajira Afrika

Kamisheni ya UM juu ya Maendeleo ya Uchumi kwa Afrika (ECA) imewasilisha ripoti mpya Geneva inayotathminia hali ya uchumi, kwa ujumla, barani Afrika kwa 2009. Mada ya ripoti inasema: "Tuendeleze Kilimo Afrika kwa Fungamano za Maadili ya Kikanda".

Kwa mujibu wa ripoti, matatizo ya kifedha yaliojiri duniani katika kipindi cha karibuni, ikichanganyika na mzoroto wa kiuchumi, yamepunguza mahitaji ya bidhaa za Afrika katika soko la kimataifa, na kusababisha mporomoko, wa kima kikubwa, kwenye bei za bidhaa zinazosafirishwa nje. Ripoti ilitilia mkazo umuhimu wa mataifa ya KiAfrika kuwekeza fedha za maendeleo kwenye huduma za kilimo, ilivyokuwa bara la Afrika hutegemea zaidi sekta hii "kuzalisha ajira, ukuaji imara wa uchumi, mapato ya fedha za kigeni na pia mapato ya kodi." Ripoti ilitayarishwa bia na Kamisheni ya ECA pamoja na Kamisheni ya Umoja wa Afrika.