Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Asubuhi, Baraza la Usalama lilifanyisha mkutano kusailia hali katika Bosnia na Herzegovina. Wajumbe wa Baraza walipatiwa fafanuzi juu ya maendeleo ya kurudisha “utulivu na usimamizi wa utawala wa muda mrefu” kieneo, kutoka Mjumbe Mkuu mpya wa UM kwa Bosnia na Herzegovina, Valentin Izko. Alisema hali katika miezi sita iliopita nchini Bosnia-Herzegovina ilikuwa “imara na isio wasiwasi” lakini umoja wa taifa, katiba na mfumo wa kiTaifa ni masuala ambayo bado yanaendelea kupigwa vita na Republika Srpska, eneo la nchi ambalo limeashiria linataka haki ya kujiamulia wenyewe na kujitenga. Na mnamo alasiri Baraza la Usalama lilifanyisha kikao rasmi juu ya ziara ya karibuni ya wajumbe wa Baraza katika JKK, Rwanda, Liberia na Ethiopia, ambapo walipata fursa ya kushauriana na wawakilishi wa Umoja wa Afrika (UA).

Asubuhi, Baraza la Usalama lilifanyisha mkutano ili kusailia hali katika Bosnia na Herzegovina. Wajumbe wa Baraza walipatiwa fafanuzi juu ya maendeleo ya kurudisha "utulivu na usimamizi wa utawala wa muda mrefu" kieneo, kutoka Mjumbe Mkuu mpya wa UM kwa Bosnia na Herzegovina, Valentin Izko. Alisema hali katika miezi sita iliopita nchini Bosnia-Herzegovina ilikuwa "imara na isio wasiwasi" lakini umoja wa taifa, katiba na mfumo wa kiTaifa ni masuala ambayo bado yanaendelea kupigwa vita na Republika Srpska, eneo la nchi ambalo limeashiria linataka haki ya kujiamulia wenyewe na kujitenga. Na mnamo alasiri Baraza la Usalama lilifanyisha kikao rasmi juu ya ziara ya karibuni ya wajumbe wa Baraza katika JKK, Rwanda, Liberia na Ethiopia, ambapo walipata fursa ya kushauriana na wawakilishi wa Umoja wa Afrika (UA).