Mkutano wa BK kuzingatia matatizo ya uchumi na fedha duniani waakhirishwa

27 Mei 2009

Ijumanne asubuhi, kwenye kikao cha wawakilishi wote wa Baraza Kuu (BK) la UM, kulichukuliwa uamuzi wa pamoja wa kuakhirisha Mkutano Mkuu juu ya Migogoro ya Uchumi na Fedha Duniani na Athari Zake Dhidi ya Maendeleo, kikao ambacho kilitarajiwa kifanyike baina ya Juni 1 hadi 03.

Tarehe mpya ya Mkutano sasa hivi itakuwa kuanzia Juni 24 mpaka 26. Raisi wa kikao cha 63 cha Baraza Kuu, Miguel d'Escoto Brockmann aliwaambia wajumbe wa kimataifa kwamba alilazimika kusogeza tarehe ya mkutano kwa sababu ya kuselelea kwa matatizo ya fedha na kiuchumi kimataifa kwa sasa, na kwa kuambatana na ombi la Mataifa Wanachama pamoja na taasisi za UM, zilizopendekeza kwanza kupatikane ratiba ya kuridhisha kwa wote ili kuhakikisha maafikiano yataupatia umma wa kimataifa suluhu yenye natija kwa wote pote ulimwenguni.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter