Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICRC inasema vita, maafa ya kimaumbile na bei ya juu ya chakula yaendelea kudhuru umma masikini duniani

ICRC inasema vita, maafa ya kimaumbile na bei ya juu ya chakula yaendelea kudhuru umma masikini duniani

Ripoti ya 2008 Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC) iliowakilishwa mjini Geneva wiki hii na mkuu wa taasisi hiyo, Jakob Kellenberger, ilibainisha kwamba mamilioni ya watu walioathirika na hali ya mapigano duniani, waliendelea kumedhurika zaidi kimaisha kwa sababu ya mchanganyiko wa athari za vita, maafa ya kimaumbile na kupanda kwa bei za chakula kwenye soko la kimataifa.

Alitoa mfano wa mataifa ya Afghanistan, Usomali na Pakistan, ambayo alisema yalishuhudia "maisha magumu zaidi kwa umma wao, watu ambao tangu hapo awali walisumbuliwa na athari haribifu za vita na mapigano, pamoja na ukali wa madhara yalioletwa na maafa ya kimaumbile na bei ya juu ya chakula."