Skip to main content

UM unajiandaa kufungamanisha teknolojiya ya ICT na huduma za kufyeka hali duni

UM unajiandaa kufungamanisha teknolojiya ya ICT na huduma za kufyeka hali duni

Maofisa wa UM wamekutana leo mjini Geneva, Uswiss pamoja na wavumbuzi wa mawasiliano ya kompyuta kwa majadiliano ya kuzingatia taratibu za kuyasaidia mataifa yanayoendelea, kujiunganisha na matumizi ya mitandao ya mawasiliano ya kisasa ya kompyuta ulimwenguni.