IFRC inabashiria kuongezeka karibuni kwa wagonjwa wa kipindupindu Zimbabwe
Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC), linabashiria mnamo siku chache zijazo jumla ya watu walioambukizwa na maradhi ya kipindupindu katika Zimbabwe itafikia 100,000.