Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasomali 67,000 wang'olewa makazi Mogadishu na mapigano

Wasomali 67,000 wang'olewa makazi Mogadishu na mapigano

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti jumla ya raia wa Usomali wanaokimbia mapigano yaliokithiri, kwa nguvu, mnamo siku za karibuni kwenye mji mkuu wa Mogadishu na maeneo jirani, sasa hivi, imekiuka wahamiaji 67,000.