Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya ukatili dhidi ya raia katika majimbo ya JKK kuitia wasiwasi UNHCR

Hali ya ukatili dhidi ya raia katika majimbo ya JKK kuitia wasiwasi UNHCR

Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR), kutokea Geneva, amesema UM una wasiwasi na ripoti ilizopokea juu ya kuendelea kwa vitendo vya ukatili, ikichanganyika na matumizi mabaya ya mamlaka pamoja na unyanyasaji dhidi ya raia katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini katika JKK.

Vitendo hivi imeripotiwa huendelezwa na wafuasi wa makundi haramu ya waasi, na baadhi ya wanajeshi wa serikali, hali ambayo tangu mwezi Januari iliwalazimisha wakazi wa maeneo hayo kuyahama mastakimu ili kunusuru maisha. UNHCR inaihimiza Serikali ya JKK, kwa kusaidiwa na jumuiya ya kimataifa kuupatia umma raia hifadhi na ulinzi unaofaa dhidi ya vitendo hivyo karaha.