Baraza la WHO lahitimisha mkutano wa mwaka Geneva

Baraza la WHO lahitimisha mkutano wa mwaka Geneva

Mkutano wa mwaka wa Baraza Kuu la Shirika la Afya Duniani (WHO) umemaliza kikao cha 2009 Ijumaa ya leo, kikao ambacho Mkurugenzi wa WHO, Dktr Margaret Chan alisema kilifanikiwa kuwapatia walimwengu “bishara ya nguvu ya masharti ya kudumu kuhusu maamirisho ya miradi ya afya ya jamii” pote ulimwenguni.

Aliseema tatizo la afya lilioukaba ulimwengu, kwa sasa hivi, ni lile la maambukizi ya kasi ya vimelea vya homa ya mafua ya A(H1N1). Alihadharisha umma wa kimataifa kuwa macho ili kujikinga na hatari ya kutapakaa kwa vimelea hivyo na kuathiri mataifa ya Kusini ya Dunia, ambayo yameepukana na maambukizi ya homa hiyo kwa hivi sasa. WHO inatarajia mnamo wiki zijazo, mripuko wa homa hii mpya ya mafua ya H1N1 utaendelea kusambaa kwenye mataifa mapya, na ndani ya ya katika yale mataifa yaliokwisha kudhurika nayo.  Kwa mujibu wa WHO, kuanzia asubuhi ya Ijumaa ya leo, nchi 42 zimeripoti rasmi jumla ya wagonjwa 11,168 walioambukizwa na vimelea vya homa ya mafua ya H1N1, ikjumlisha vifo 86.