Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UNAMID atoa mwito kwa Chad na Sudan kusitisha, halan, mapigano mipakani

Mjumbe wa UNAMID atoa mwito kwa Chad na Sudan kusitisha, halan, mapigano mipakani

Rodolphe Adada, Mjumbe Maalumu wa Pamoja wa UM/UA kwa Darfur, UNAMID ametoa taarifa maalumu yenye mwito unayoyataka mataifa jirani ya Chad na Sudan kukomesha, halan, mapigano yalioshtadi karibuni katika eneo la mpakani.

Alizitaka nchi hizi "kujizuia na vitendo vya uchokozi ambavyo huenda vikapalilia hali ya wasiwasi, na kuzidisha mateso kwa raia katika Darfur, hususan miongoni mwa wahamiaji wa ndani (IDPs) na wale wa kutoka nchi jirani." Adada anakhofia hali ya wahka iliojiri baina ya Chad na Sudan kwa sasa inahatarisha kuharibu zile jitihadi za kuleta amani ya kudumu kwa umma wa Darfur.