Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wahajiri mastakimu Mogadishu inaendelea kufurika

Idadi ya wahajiri mastakimu Mogadishu inaendelea kufurika

Shirika la Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti raia 45,000 ziada walihajiri mastakimu, mnamo siku 12 zilizopita, kutoka mji wa Mogadishu, Usomali baada ya kujikuta wamenaswa kwenye mazingira ya mapigano, baina ya makundi yanayohasimiana nchini, wapiganaji ambao wameripotiwa kutumia silaha za otomatiki na makombora, hasa katika yale maeneo ya kaskazini ya mji.