Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM inasema raia katika JKK wanaendelea kuteswa kihorera

UM inasema raia katika JKK wanaendelea kuteswa kihorera

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imetoa taarifa yenye kusema kuna ushahidi baadhi ya wanajeshi wa vikosi vya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (FARDC) hushiriki kwenye vitendo vya kunyanganya kwa nguvu na kunajisi kimabavu raia, na wakati huo huo kuendeleza mauaji ya raia, halkadhalika, katika eneo la kaskazini-mashariki ya nchi.

Kwa mujibu wa taarifa ya OCHA makosa haya ya jinai vile vile yaliendelezwa na makundi ya waasi, mathalan, lile jeshi la mgambo la Wahutu katika JKK la FDLR. Askari wa jeshi la taifa Kongo la FARDC walishtakiwa kuchukua ngawira kutoka kwa raia, kunyanganya mavuno na kubomoa nyumba za watu kihorera, pamoja na vitendo karaha vya kunajisi watu kimabavu.