Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM amemchagua raisi mstaafu wa Marekani kuwa Mjumbe Maalumu kwa Haiti

KM amemchagua raisi mstaafu wa Marekani kuwa Mjumbe Maalumu kwa Haiti

Raisi mstaafu wa Marekani, W. J. Clinton ameteuliwa na KM leo hii, kuwa Mjumbe Maalumu wa UM kwa Haiti.

Raisi Clinton ana uhusiano mkubwa na mataifa ya maeneo ya Karibiani. Kwenye taarifa ya uteuzi huo KM alimpongeza Raisi Clinton na anaamini atachangisha pakubwa kwenye zile jitihadi za kuihamasisha jumuiya ya kimataifa kuisaidia Haiti kufufua tena uchumi wa taifa na ujenzi wa amani nchini, maendeleo yatakayobashiria natija za muda mrefu kwa umma wote muhitaji wa taifa hili la Karibiani.