Wahusika wingi wanatakikana kutekeleza sera za kupunguza silaha duniani, anasema KM

19 Mei 2009

Wajumbe wa kimataifa wanaohudhuria Mkutano wa Upunguzaji Silaha Geneva, walinasihiwa na KM Ban Ki-moon kwamba kunahitajika kuwepo mwelekeo unaohusisha pande mbalimbali pindi wamewania kuwasilisha kidhati maendeleo yanayosarifika kwenye zile juhudi za kupunguza silaha duniani.

Alisema "tunaishi kwenye ulimwengu wa kutegemeana" na alitoa mfano juu ya namna mizozo ya karibuni ya chakula, nishati na uchumi yalivyoathiri kila taifa ulimwenguni, migogoro ambayo, alisisitiza, ilihitajia "ushirikiano mpya miongoni mwa wahusika mbalimbali wa kimataifa" kuitatua.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter