Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiongozi wa waasi Darfur amejisalimisha kwa ICC

Kiongozi wa waasi Darfur amejisalimisha kwa ICC

Kiongozi wa kundi la waasi wa Darfur, anayeitwa Bahar Idriss Abu Garda, Ijumapili aliwasili Uholanzi, kujisalimisha, kwa khiyari, kwa Mahakama ya Kimataifa Juu ya Jinai ya Halaiki (ICC).

Abu Garda ni mmoja wa makamanda watatu walioripotiwa kuongoza waasi 1,000 walioshambulia kambi ya Haskanita iliopo Darfur Kusini, dhidi ya vikosi vya ulinzi amani vya UA katika Sudan (AMISOM), mnamo tarehe 29 Septemba 2007 na kuua wanajeshi 12 pamoja na kujeruhi askari wanane wengine. Vikosi vya AMISOM vilikabidhiwa madaraka ya kulinda amani wakati huo, kabla ya vikosi vya mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) kuwasili kwenye eneo. Mnamo Novemba 2008, Luis Moreno-Ocampo, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya ICC, aliwakilisha ushahidi ambao alisema umethibitisha Abu Garda na makamanda wawili wengine wa makundi ya waasi, walishiriki katika "kutayarisha na kuongoza vikosi vya majeshi yao ya mgambo, yaliohujumu kambi za AMISOM ambazo waliziharibu, kwa ukamilifu, ikijumlisha mali na majumba, tukio ambalo liliathiri sana huduma za kugawa misaada ya kiutu na kuimarisha usalama wa mamilioni ya wakazi wa Darfur waliohitajia ulinzi wa vikosi vya kimataifa." Mwendesha Mashitaka Moreno-Ocampo anaamini makamanda watatu watuhumiwa wanahusika na makosa matatu ya jinai ya vita. Mtuhumiwa aliyejisalimisha kwa khiyari, Bahar Idriss Abu Garda, anatoka kabila ya Zaghawa ya Sudan, na alifikishwa mahakamani Ijumatatu ambapo alikana makosa. Abu Garda ni atakuwa mtu wa kwanzaanayehusika na mgogoro wa Darfur kukabili Mahakama ya ICC, kwa khiyari.