Skip to main content

Kamishna wa Haki za Binadamu aisihi Marekani kushtaki waliotesa watuhumiwa ugaidi

Kamishna wa Haki za Binadamu aisihi Marekani kushtaki waliotesa watuhumiwa ugaidi

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay ametangaza kukaribisha uchaguzi wa Marekani kuwa mwanachama mpya wa Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu.

Kufuatia tukio hilo Pillay ametoa taarifa yenye kumsihi Raisi wa Marekani Barack Obama kufungua mashtaka mapya, dhidi ya wale raia waliotuhumiwa kutesa, na kushiriki kwenye udhalilishaji na kashfa nyengine zilizokiuka haki za kiutu dhidi ya watuhumiwa ugaidi, kwa niaba ya watawala, katika miaka ya karibuni. Kwenye insha alioiandika na kuchapishwa kwenye gazeti la International Herald Tribune, Pillay alisema Marekani inawajibika kuchunguza vitendo vya kuhamisha watu waliotuhumiwa ugaidi na kupelekwa kuteswa kwenye magereza ya siri yaliotawanyika katika sehemu mbalimbali za dunia. Alinasihi kwamba watesaji wa watuhumiwa ugaidi ni lazima wafikishwe mahakamani kukabili haki, kwa sababu vitendo vyao vilikiuka na kutengua kanuni za kimataifa za kupiga marufuku mateso.