Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UNEP inahimiza mapinduzi ya kilimo Afrika kidharura kunusuru umma njaa

Ripoti ya UNEP inahimiza mapinduzi ya kilimo Afrika kidharura kunusuru umma njaa

Ripoti mpya ya Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) imeyanasihi mataifa ya Afrika kujihusisha haraka kwenye ile miradi ya lazima, inayohitajika kuleta mapinduzi ya sekta ya kilimo, mageuzi yatakayousaidia umma, kwa ujumla, kupata chakula maridhawa na pia kuwanusuru na hatari ya miripuko ya hapa na pale ya sera za kigeugeu za chakula katika soko la kimataifa.