Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mshauri wa misaada ya dharura ahadharisha mapigano ya kikabila Sudan Kusini yanahatarisha amani

Mshauri wa misaada ya dharura ahadharisha mapigano ya kikabila Sudan Kusini yanahatarisha amani

Lise Grande, Naibu Mratibu Mkaazi wa UM juu ya Misaada ya Kiutu Sudan Kusini ameeleza kuwa na wahka mkuu juu ya mapigano yaliozuka tarehe 08 Mei (2009), kitambo tu baada ya John Holmes, Naibu KM wa UM juu ya Misaada ya Dharura kumaliza ziara yake Sudan Kusini hivi juzi.

Mapigano haya yalizuka baina ya makabila ya Lou Nuer na Jikany na kusababisha vifo vya watu 60 ziada, ikijumuisha wanawake, watoto na wanaume kwenye kijiji cha Torkech katika Wilaya ya Nasir. Watu 1,550 wengine waling'olewa makazi kutokana na mapigano haya. UM imetuma timu maalumu kufanya uchunguzi wa tukio hili, na umetoa mwito unaopendekeza kwa viongozi wa jamii zinazohasimiana, pamoja na wakuu wenye mamlaka kusuluhisha mgogoro wao kwa njia za amani.