Mjumbe wa UM kwa Usomali ashtumu mashambulio ya Mogadishu dhidi ya serikali

12 Mei 2009

Mjumbe Maalumu wa UM kwa Usomali, Ahmedou Ould- Abdallah ameshtumu vikali kuendelea kwa mashambulio dhidi ya wawakilishi wa Serikali halali ya Usomali na uhariibifu wa mali za serikali unaofanyika kwenye mji wa Mogadishu.

Vitendo hivi vilivyosababisha vifo kadha vya raia na kulazimisha idadi kubwa ya raia kuhama makwao ni hali isiokubalika abadan, alisema. Ould-Abdallah pia alikumbusha Mpango wa Amani wa Djibouti ndio mfumo wa kufuatawa na makundi yote yaliowania kidhati kurudisha usalama na amani ya eneo lao. Alisema anaamini mamshambulio haya yanayofanywa na wapinzani "yanaungwa mkono na wageni" wenye dhamira ya kuchukua serikali kwa nguvu. Alisihi hali hi lazima isite, halan!

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter